Wanawake Same waamua kutumia fursa za utalii.Watangaza utalii wa Mkomazi kama mbuga inayotegemea kukua kwa kasi.
Mpango mkakati wa Utalii wa Wilaya umekuwa dira kwa wadau kushiriki.Ni wa miaka mitano(5).
Kamishna wa TANAPA kanda aliyemwakilisha Mkurugenzi wa utalii bi.Dora Aloyce aeleza jinsi Mkomazi walivyojipanga kuongeza watalii kwa kutenga eneo maalum kwa utalii wa faru,litaanza karibuni.
Wananchi Same wasema wako tayari kwa utalii.Waazimia kuanza na utalii wa ndani.Zaidi ya watu 300 wajitokeza siku hiyo.
DC Same Mhe.Rosemary Senyamule aongoza kundi hilo na kuiomba Wizara ya Utalii kuwaunga mkono ili mbuga hii iweze kuwa na faida kwa serikali na kwa wananchi.Awashukuru kwa ushirikiano unaoendelea.
"Rais wetu Mhe.Dr.John Pombe Joseph Magufuli amesema utalii ni kati ya vipaumbele vyetu mwaka huu.Sisi sote tunamuunga mkono kwa vitendo".Asema DC huyo.
DC awashukuru wanawake na wananchi wote kwa kushiriki na kuwa sasa iwe ni mwanzo wa kila mwisho wa wiki kutembelea vivutio vyetu.
Awashukuru wadau kuanza kutekeleza mpango mkakati kwa kuanzisha duka la vitu vya asilina kuleta gari la kisasa kwa ajili ya utalii ambavyo vilizinduliwa siku hiyo.
Awakaribisha wote kutembelea Utalii Same kwani gharama ni nafuu na vivutio ni vya kiwango cha juu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.