Halmashauri ya Wilaya ya Same,Mkoani Kilimanjaro imezindua mnada na soko la barabarani katika eneo la Kirinjiko kwa lengo la kuongeza mapato na kuwawezesha wananchi watakaofika katika Hospitali mpya ya Wilaya iliyo jirani na eneo hilo pamoja na wasafiri kupata huduma katika mnada huo.
Mnada huo ulizinduliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bi.Kasilda Mgeni Mapema mwezi Septemba mwaka huu ambapo aliwahimiza wananchi wa Same kutumia vema fursa hiyo katika kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza katika Uzinduzi huo kuu wa Wilaya ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Soko ambao umekamilika kwa awamu ya kwanza .
“Ndugu zangu wafugaji wa Wilayah ii ya Same na Wilaya za jirani niseme tuu kwamba Mnada huu ni wa kwenu,Serikali imewajali kwa kuwajengea mnada huu, hivyo muutumie vizuri na kutunza miundombinu iliyopo” alisema Mkuu huyo.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Same alisema kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022 inaonyesha Wilaya ya Same ina jumla ya Ng’ombe laki moja na tatu, Mbuzi laki moja na kumi na saba elfu kondoo sabini na tatu elfu na sita themanini na nne.
“Tumeanzisha mnada huu kama fursa ya kiuchumi kwa wafugaji na wananchi wengine wa Same lakini pia mnada huu pamoja na soko la barabarani ni huduma kwa wananchi wa Same na hata wasafiri wanaotumia barabara ya Same-Dar es Salaam” alisema Mhe.Kasilda
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya aliwataka wafugaji kujenga tabia ya kupunguza mifugo kwa kuiuza wakati wa kiangazi ambapo malisho ni haba na kununua mingine pale kiangazi kinapokwisha ili kuepuka hasara ya mifugo kufa kwa kukosa malisho.
Akizungumza katika Uzinduzi huo Mkurugenzi wa Wilaya ya Same Bi. Anastazia Tutuba alisema Wilaya imejitahidi kuhakikisha kwamba huduma zote muhimu zinapatikana katika eneo hilo ili kuwawezesha wafanyabiashara kutumia vema eneo hilo.
“Hapa kuna huduma ya Umeme,maji,vyoo na hata barabara za eneo hili ni za uhakika na tayari tumeshagawa maeneo zaidi ya 500 ya kujenga vibanda vya biashara na kuchomea nyama”alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Same Mhe. Yusto Mapande alisema lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanajikwamua kiuchumi hivyo soko hilo litasaidia kukuza uchumi wa Wananchi.
“Jambo ambalo wananchi wanalitarajia kutoka kwaviongozi wao ni kuwaonyesha njia ambayo itatatua matatizo yao ikiwa kuwaletea fursa ya ajira na fursa za kiuchumi na katika eneo hili hadi sasa kuna ajira zaidi ya mia sita”alisema Mapande
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.