Waziri wa madini Mhe.Angela Kairuki amepeleka neema ya misaada ya kibinadamu kwa waathirika 7,000 wa maafuriko pangani na bwawa la nyumba ya Mungu katika wilaya ya Same ambao wanaishi katika kambi za muda za Rolesho, Marwa na Bagamoyo.
Kairuki alikwenda jana katika kambi hizo zenye kaya 980 kwa ajili ya kukabidhi misaada yenye thamani ya Tsh. Milioni 12 akiwa ameongozana na Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jaseen Al-Najem.
Mafurikio hayo yalitokea mwezi mei mwaka huu, baad aya sehemu ya kupumulia ya Bwawa la Nyumba ya Mungu kujaa maji kupita kiwango chake na kusabababisha hayo kujaa kiwango cha juu ya wastani na kisha kumwagika mitaani kupitia mto Pangani.
"Mimi ni mzaliwa wa Same nakuja kwetu hapa na Mheshimiwa Balozi wa Kuwait ni kwasababu tumeguswa sana na hali mliyo nayo kwasasa na tukaona tuje tuwafariji baada ya kutokea mafuriko ambayo yaliharibu kabisa makazi yenu, mali na mazao ya chakula na biashara" alisema Mhe. Kairuki.
"Baada ya kuguswa na jambo hili, nikaona ni vizuri kama mzawa nije kuungana nanyi kwa kuwapa misaada mbalimbali ambayo itawafariji katika hiki kigumu, nimewaletea mablangeti 350 na maturubai ya kuzungushia nyumba yapatayo mia mbili (200), " alisema Mhe.Kairuki.
Waziri Kairuki alisema Balozi Al-Najem amemuunga mkono katika kuwafariji waathirika hao baada ya kusoma taarifa za mahitaji ya binadamu yanayohitajika katika kambi hizo pamoja na hali waliyo nayo kwa sasa.
Vijiji vilvyoathiriwa na mafuriko hayo yaliyotokea mwezi Mei mwaka huu ni Marwa, Jitengeni, Kombo na Ruvu ambavyo vipo ukanda wa chini karibu na mto Pangani. Kwa upande wake Balozi Al-Najem alisema kwa kuwa Tanzania na Kuwait ni ndugu katika maswala ya kidiplomasia wana wajibu wa kusaidiana katika shida na raha,.
Kuwait imetoa tani saba za vyakula mbalimbali ikiwemo mchele, sukari unga na maharage kwaajili kuzisaidia familia za waathirika wa mafuriko hayo.
"Nimesikia bado waathirika hawa wanahitaji msaada, naahidi kwamba Kuwait itaendelea kutoa misaada mbalimbali kulingana na matakwa ya shirika la Msalaba mwekundu la Kuwait ambalo nitaelekeza lilete misaada mbalimbali kama chakula, mahema na dawa," alisema Balozi Al-Najem.
Baada ya makabidhiano hayo mkuu wa wilaya ya Same Mhe.Rosemary Staki alisema tayari serikali imetenga eneo jipya la makazi ya kudumu kwa ajili ya kuwahamisha wahanga waliohifadhiwa katika kambi za muda.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.