Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki ametembelea mabanda ya Maonesho ya mazao ya Misitu yaliyopo kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Same ukiwa ni kuelekea kilele cha Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa Machi 21,2024.
Mhe. Kairuki ameipongeza Wizara pamoja na Wadau wa misitu waliojitokeza kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu majukumu yanayotekelezwa na taasisi zao ikiwemo elimu ya uhifadhi pamoja na kuonesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na mazao ya misitu.
Pia Waziri ametumia fursa hiyo kuwataka wakazi wote wa Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro pamoja na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kutembelea maonesho hayo.
Amesema maonesho hayo ni muhimu kwao kwani wataweza kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo elimu ya ufugaji nyuki kibiashara pamoja na kujua fursa mbalimbali zinazopatikana katika mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu.
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji miti Kitaifa hufanyika kila mwaka Machi 21ambapo kwa mwaka huu Tanzania inaadhimisha Kilele hicho kwa kupanda miti pamoja na kutembelea maonesho ya bidhaa mbalimbali zitokanazo na misitu na nyuki.
Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Misitu Duniani na siku ya upandaji Miti Kitaifa yatafanyika Wilayani Same Machi 21 mwaka huu na Mgeni Rasmi atakua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Isdor Mpango.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.