Wauguzi Wilayani Same wametakiwa kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia weledi wa kazi yao ikiwa ni pamoja na kutunza siri za Wagonjwa.
Wito huo ulitolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dk.Alex Alexander wakati akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani.
Maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani hufanyika Mei 12 ya kila mwaka ambapo Wauguzi hukutana kwaajili ya kukumbushana majukumu yao.
Dk.Alexander alisema Wauguzi pamoja na madaktari wana jukumu kubwa la kushughulika na uhai wa binadamu hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa kujituma na kuhakikisha kuwa mgonjwa anayepatiwa huduma anaondoka akiwa ameridhika na huduma aliyopatiwa.
"Wauguzi na madaktari tunakutana na mambo mengi wakati wa kutimiza majukumu yetu hivyo tunapaswa kulinda siri za watu tunaowahudumia"alisema
Daktari huyo alisisitiza Wauguzi pia kuwa waaminifu na waadilifu wakati wakitekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wagonjwa.
Akizungumzia historian ya maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani,Muuguzi Aramica Mangi wa Hospitali ya Wilaya ya Same alisema siku hiyo huazimishwa Kama kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Muuguzi Florence Nightingale ambaye ndiye muasisi wa fani ya Uuguzi Duniani.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.