Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasild Mgeni, amevitaka vikundi vya wanawake,vijana na walemavu ambavyo vinadaiwa mikopo ya asilimia 10 kuhakikisha kwamba wanarejesha mikopo hiyo ili iweze kutolewa kwa wahitaji wengine.
Mhe. Kasilda ametoa wito huo wakati akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vilivyonufaika na mkopo huo ambapo alisema ucheleweshaji wa kurejesha mikopo hiyo unakwamisha maendeleo ya Wilaya kwani Halmashauri inashindwa kuendelea kukopesha.
Amesema ni muhimu kwa wajasiriamali kuhakikisha wanarudisha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwezesha mfumo wa mikopo kuendelea kuwasaidia wengine na hata wao kukopa tena pale wanapohitaji kufanya hivyo.
“Urejeshaji wa mikopo kwa wakati ni muhimu kwa ustawi wa kiuchumi wa vikundi vya wajasiriamali na pia kuhakikisha upatikanaji wa mikopo zaidi kwa ajili ya kupanua biashara zenu na kuboresha maisha yenu” alisema.
Akizungumza kwenye kikao hicho Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw. Charles Anatoly alisema jumla ya vikundi 344 vya wajasiriamali vinadaiwa zaidi ya shilingi milioni 300 ambapo alisema kwa mwaka huu wamefanikiwa kupokea marejesho ya shilingi milioni 37.
“Tunaendelea kufuatilia marejesho ya haya madeni na yanaendelea kulipwa japo kwa taratibu sana,tunaendelea kuvikumbusha vikundi viendelee kulipa,na ambavyo vitakiuka hatua Zaidi zitachukuliwa” alisema Bw. Anatoly.
Mkuu huyo ametoa miezi mitatu wa vikundi hivyo kuhakikisha kuwa ifikapo mwezi Desemba 2024 madeni yote yanatakiwa yawe yamesharejeshwa kikamilifu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.