Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Same Bi.Anna-Claire Shija akiwa mgeni rasmi katika mafunzo kwa wataalamu wa afya juu ya DHFF,JAZIA na ICHF iliyoboreshwa na matumizi ya mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa katika vituo vya kutolea huduma kwa siku tatu aliwaasa watalam hao kuzingatia mafunzo hayo kwani ni muhimu sana katika ugatuaji wa mipango,bajeti na matumizi sahihi ya fedha zinazotumwa na Serikali moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma ya afya.
Halmashauri ya wilaya ya Same kwa kushirikiana na wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na HPSS (health promotion systems strengthening) wameendesha mafunzo hayo kwa wataalam wa afya katika ukumbi wa RC Wilayani Same.
Aidha Bi.Anna-Claire Shija aliwataka wataalam wa afya kuzingatia maadili ya kazi na kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na weledi ili kuleta tija katika utendaji wa shughuli zao na kuiletea maendeleo wilaya ya Same.
Mwisho Bi.Anna-Claire Shija aliwahamashisha wataalam hao kupenda kazi yao na kuipenda wilaya ya Same na kusema “Same itajengwa na sisi wenyewe hakuna mtu mwingine atakayeijenga Same ila ni sisi wenyewe"
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.