Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi. Anastazia Tutuba amesema Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya tahadhari ya mafuriko kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ili kuepuka madhara yanayoweza kutokana na mvua za Elnino.
Kwa mujibu wa Taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) mvua za Elnino zinatarajia kunyesha hadi mwishoni mwa mwezi Februari 2024.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Mkurugenzi huyo alisema tayari Kamati za kukabiliana na maafa zimeshaundwa kuanzia ngazi ya Vitongoji,Vijiji na Kata na tayari zimeshapewa maelekezo kuhusu hatua za kuchukua pale hali inapokua ya kuhatarisha.
"Swala la majanga ya mafuriko linadhibitiwa kuanzia ngazi ya Kitongoji, Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa mpaka Taifa, hivyo sisi kama Halmashauri tayari tumeunda Kamati za maafa ambazo kwa sasa zinaendelea kutoa elimu juu na namna ya kujikinga na Maafa"alisema Bi.Tutuba
Alisema katika Wilaya ya Same kuna maeneo hatarishi ambayo hata kipindi cha Mvua za kawaida za masika hukumbwa na mafuriko hivyo wananchi walishaelekezwa kuhama kwa muda katika maeneo hayo.
Aliyataka maeneo ambayo hukumbwa na adha ya ya mafuriko katika Wilaya ya Same kuwa ni Hedaru,Makanya,Kisima,Ruvu,Njoro na maeneo mengine ambayo hupata majanga ya maporomoko ya miamba ni Myamba,Msindo,Vunta na Mtii.
"Kwa kipindi hiki cha Mvua za Elnino ni vema wananchi wakaepuka kukaa chini ya miti,waepuke kupita na vyombo vya Moto maeneo yenye maji mengi,wasiguse nyaya za umeme popote wanapoziona,lakini wanatakiwa pia kuwa na namba za viongozi wao ili hata majanga yanapotokea waweze kutoa taarifa ili wapate msaada wa haraka" alisema.
Akizungumzia suala hilo Diwani wa Kata ya Ruvu Mhe.Yaigongo Mrutu alisema Kata ya Ruvu ni miongoni mwa Kata ambazo husumbuliwa na adha ya mafuriko hivyo akaiomba Serikali ya Wilaya kutoa msaada wa haraka pale utakapohitajika.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.