Wakulima wa Kahawa Wilayani Same wameshauriwa kubadilika kutoka kutumia mbegu za zamani ambazo zinachelewa kukomaa na kuanza kutumia mbegu zilizoboreshwa za Arabica Compact.
Akizungumza kwenye maonesho ya Nane nane Kanda ya Kaskazini Mshauri wa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Fidel Bigula amesema mbegu ya Arabica Compact ni mbegu mpya ambayo inazaa ndani ya miaka mitatu tangu ioteshwe na inazaa sana kuliko mbegu za zamani.
“Mbegu hii imeboreshwa na watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kahawa TACRI ambapo tangu imeanza kusambazwa imeonyesha mafanikio kwa wakulima” alisema
Alisema kwa Wilaya ya Same Tayari mbegu hiyo imesambazwa katika Kata mbalimbali na inaendelea kusambazwa ili kuhakikisha wakulima wote wanaachana na mbegu za zamani ambzo zina gharama kubwa ya kuzihudumia na uzao wake ni mdogo.
Bw.Bigula alisema mbegu ya Arabica Compact hutoa hadi kilo tano katika mchumo mmoja tu kwenye shina moja wakati mchumo mmoja wa mbegu za asili haufiki hata kilo tatu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.