Kikao cha kuimarisha uhusiano kati ya serikali,taasisi za dini na taasisi zisizo za serikali(NGOs) chafanyika wilayani Same.
Serikali yaeleza miradi iliyofanyika 2018 kitaifa na wilayani.Waeleza mipango ya wilaya 2019,wajadili utekelezaji wa mpango mkakati wa mazingira na utalii.
Viongozi wa dini/NGOs wapongeza serikali ya awamu ya tano kwa kasi kubwa ya miradi na maendeleo.Mradi wa maji wawafurahisha zaidi.Waahidi ushirikiano wa dhati pamoja na kumuombea Mhe.Rais na serikali yake.
Naibu Waziri mambo ya ndani Mhe.Masauni apewa salamu za Mhe.Rais,awahimiza viongozi kudumisha amani.Afurahishwa na mpango huu wa kushirikisha wadau wajue yanayofanywa na serikali.
Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Same awashukuru kufanikisha amani,miradi,elimu,mazingira,maji,afya na yote yaliyowezesha Wilaya kupiga hatua haraka.Waweka maazimio 12 ya kushirikishana 2019 kwa maendeleo ya Wilaya.Waomba utaratibu huu uendelee.
Wafanya maombi maalum ya kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr John Pombe Magufuli.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.