Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Same Mhe.Isaya Mngulu ameongoza kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2021,ambapo kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Edward Jonas Mpogolo,viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya na wajumbe wa chama kutoka kata 34 za wilaya ya Same.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Same Bi.Anastazia Tutuba pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri,hali kadhalika idara za Serikali ambazo ni TANESCO,TARURA,RUWASA,TANAPA,NIDA,RITA ambao ndio watekelezaji na watendaji wa Ilani ya Uchaguzi.Vile vile watu wa benki za CRDB na NMB walihudhuria kikao hicho.
Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi uliwasilishwa ambapo watumishi wamepandishwa vyeo na kubadilishwa miundo ya watumishi,malimbikizo ya mishahara yamelipwa,ajira mpya za walimu na afya,sayansi,taknolojia na ubunifu kwa maana ya mifumo ya TEHAMA inatumika kutoa huduma kwa wananchi.
Utekelezaji mwingine uliofanyika ni kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji,kuwekwa kwa umeme wa REA katika kata mbalimbali,kutolewa kwa mikopo isiyo na Riba kwa wanawake,vijana na walemavu,kusajiliwa kwa wakulima 25,000 katika mfumo wa MOBILE KILIMO kwa ajili ya kutafuta masoko ya bidhaa zao,kujengwa kwa miundombinu ya barabara,vyeti vya kuzaliwa na vifo kutolewa,wananchi kupata vitambulisho vya Taifa(NIDA) pamoja na wananchi kupata mafunzo na mbinu za kujikinga na wanyamapori hatari Tembo.
Wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi waliridhia na kuipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
"Kwa Kishindo Tunatekeleza"
CCM Hoyeeeeeee!!
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.