Utalii wa asili waleta Maktaba kata ya Mshewa wilayani Same ambapo kukuza Utalii wa asili ni moja ya malengo yaliyopo kwenye mpango mkakati wa kukuza utalii wilayani Same.Wageni wengi wameanza kuufurahia na kutembelea vivutio vya asili,maporomoko ya maji,mapango,mashamba,mabwawa,misitu,milima na vingine.
Watalii toka Uingereza kupitia shirika la World Expedition Exchange waliotembelea kijiji cha Goma kata ya Mshewa walitoa vitabu ili kuunga mkono juhudi za Serikali juu ya elimu.Vitabu hivyo viliwezesha kuanzisha maktaba katika kijiji hicho itakayotumiwa na wanafunzi wa kata ya Mshewa na kuongeza maarifa.Idadi kubwa ya vitabu hivyo ni vya masomo ya sayansi.
Ndugu Elly Kimbwereza ambaye alikuwa mwenyeji wa wageni hao alieleza jinsi utalii wa asili unavyoweza kuunganishwa na shughuli za jamii husika na kuleta maendeleo kwa haraka kwani watalii wengine wameshashiriki kutengeneza barabara katika kijiji hicho.Alisema kwa kuwa vitabu vingi ni vya sayansi vitasaidia katika adhma ya Tanzania ya viwanda.
DC Same Mhe.Rosemary Senyamule aliyezindua Maktaba hiyo,alitoa wito kwa wananchi kujifunza na kushiriki shughuli za utalii kwani tunavyo vivutio vingi mno ambavyo vikitumika vizuri kila mtu atafaidika.Katika mpango mkakati wa Utalii,pamoja na kutaja mbuga ya wanyama Mkomazi na msitu wa Chome wenye kilele cha Shengena,wilaya imepanga kuunganisha vivutio hivyo pamoja na vivutio vya utamaduni ili Serikali na wananchi wote wafaidike na kukuza uchumi wa wilaya.
"Kuwepo kwa Maktaba hii ya kwanza kwenye kata kwa wilaya yetu kutuletea matunda mema ya kukuza elimu na ufaulu uongezeke katika kata hii"Alisema DC Same alipokuwa akiwashukuru wadau hao.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.