Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu amewataka watumishi wa Serikali na Wadau mbalimbali wa Maendeleo Mkoani Kilimanjaro kuyatumia vema matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika kuleta Maendeleo.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo Machi 11 mwaka Huu wakati akifungua Semina ya siku moja ya Usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 katika Mipango mbalimbali ya maendeleo.
Mheshimiwa Nurdin Babu alisema atahakikisha kuwa matokeo hayo ya Sensa yatatumika vema ili kuharakisha Maendeleo ya Mkoa wa Kilimanjaro katika nyanja mbalimbali.
"Matokeo haya yatumike kuweka Mipango Yote Sawa ikiwa ni pamoja na kuhuisha sera ili ziweze kutatua changamoto zilizoainishwa kwenye sensa ya 2022"alisema Mkuu wa mkoa
Alisema Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa 2022 idadi ya watu kwenye Mkoa wa Kilimanjaro imeongezeka kutoka watu 1,640,087 mwaka 2012 na kufikia watu 1,861,934 mwaka 2022.
Akizungumza katika Semina hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw.Tixon Nzunda alisema Semina hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Takwimu la Taifa (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro imejumuisha washiriki zaidi ya 500 kutoka Wilaya za Same na Mwanga.
Alisema washiriki hao ni Wakuu wa Wilaya,Makatibu Tawala wa Wilaya,Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ,Madiwani,Watendaji Kata na Vijiji,Wenyeviti wa Vijiji,Viongozi wa Dini na Viongozi wa Vyama vya Siasa.
Alisema lengo la kuwakutanisha wadau hao ni kuwajengea uwezo wa kutumia kwa usahihi matokeo ya Sensa katika kuleta Maendeleo.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.