Rais wetu Mhe.Dr John Pombe Joseph Magufuli anapambana kutufikisha katika uchumi wa kati ifikapo 2025.
"Watanzania wengi wanajiuliza Rais huyu akitoka nani ataendeleza juhudi hizi ili zisipotee!!!Jibu zuri la swali hili ni kwa watoto wa leo tukiwatunza vizuri kwa maadili na uchapa kazi.Miaka 20 ijayo ndio watakuwa watu wazima wa kuisimamia nchi yetu"Hayo yalisemwa na Mhe.Rosemary Senyamule Mkuu wa Wilaya ya Same alipokuwa akihitimisha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika wilaya ya Same.
Ilionesha kuwa swala la malezi limelegalega na kupelekea kupata watanzania wasio na uadilifu,uzalendo wala hofu ya Mungu.
Kaimu Mkurugenzi ndugu Victor Kabuje alieleza hali ya wilaya na kusisitiza haki za watoto kuzingatiwa.
NGO's zilizoshiriki siku hiyo zilieleza juhudi kubwa wanazofanya ili kuhakikisha haki za watoto zinatekelezwa.
Mhe.Senyamule aliwashukuru mahakama ya wilaya ambapo kwa mara ya kwanza mwaka huu 2019 watu wanne wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kubaka/kuwapa mimba wanafunzi.Aliwashukuru wadau wote wanaoshiriki mapambano ya kumtetea mtoto wa kike kuepusha mimba za utotoni na aliahidi kuhakikisha wahusika hao wanachukuliwa hatua.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.