Serikali imetoa Tshs 647M kwa chuo cha FDC Same ili kukarabati majengo yote pamoja na kujenga bweni,madarasa 2,jengo la utawala,karakana ya magari na darasa la chekechea.
Gharama ya ada yashuka hadi laki 250,000/= kwa mwanafunzi wa bweni.Waanzishwa mpango kwa mabinti waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali.
"Yote haya yanafanywa ili mpate ujuzi utakaowafanya mjiajiri au muajiriwe mkiwa mahiri kwenye fani zenu,pia hata mtoto wa maskini amudu ada"Alisema DC Same akiongea na wanachuo hao.
Tumieni nafasi vizuri.Amtaka mkuu wa chuo kutumia vizuri fedha hizo na mkandarasi kumaliza kazi kwa muda.Awakumbusha wananchi kutumia chuo hicho kwa kuwaleta watoto waliokosa nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha nne ili wapate ujuzi.
"Namshukuru saana Mhe.Rais Magufuli kwani chuo hiki kilikuwa kimesahaulika kwa miaka mingi mno na majengo yake yalikuwa chakavu.Lakini sasa kila kitu kitakuwa kipya.Shukrani zetu ni kukitumia vizuri"DC Same.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.