Serikali mkoani Kilimanjaro imeahidi kuwatafutia wajasiriamali masoko ya bidhaa mbalimbali wanazozalisha ili waweze kujikimu kiuchumi.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe:Kasilda Mgeni ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe:Nurdin Babu katika sherehe za kilele cha siku ya wanawake Duniani zilizofanyika kimkoa Wilayani Same.
Mhe:Mgeni alitoa ahadi hiyo baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali wanawake.
"Baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali wamenieleza kuwa changamoto yao kubwa ni masoko ya uhakika hivyo naahidi kuwa Serikali itajitahidi kutafuta masoko ya bidhaa hizi ndani na nje ya nchi"alisema Mhe:Mgeni.
Awali akitembelea banda la mjasiriamali wa viungo mbalimbali vya chakula,Halima Kilusu na mjasiriamali Catherine Wales anayetengeneza batiki wote walilalamikia kukosa masoko ya uhakika.
Wales amemuomba Mkuu wa Mkoa kuwasaidia katika kupata masoko ya uhakika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anastazia Tutuba alisema Ofisi yake itaendelea kuwawezesha wanawake wajasiriamali kiuchumi kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba.
"Tutaendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia mikopo isiyo na riba ya Halmashauri,wajiunge katika vikundi vya watu wasiopungua watano,wasajili vikundi vyao,waje kuomba mikopo"alisema Tutuba.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.