Halmashauri ya Wilaya ya Same imetoa elimu ya Afya ya Kinywa na Meno katika shule za msingi nne ili kuwawezesha wanafunzi kujua namna ya kutunza kinywa ili kuepuka maradhi ya meno.
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same Dkt.Alex Alexander wakati akieleza majukumu mbalimbali yaloyotekelezwa na Idara ya Afya.
Alisema elimu hiyo imetolewa kwenye shule za msingi za Dimbwi,Hedaru na Mbuyuni na Kisima ambapo jumla ya wanafunzi 1,400 walifikiwa na elimu hiyo.
Alisema utoaji wa elimu ya utunzaji wa kinywa na meno umefanyika kufuatia idadi kubwa ya wagonjwa wa kinywa na meno wanaofika kupatiwa huduma kwenye Wilaya ya Same.
Alisema kwa kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni,2024 jumla ya wagonjwa wa kinywa na meno 473 walihudhuria klinik kupata matibabu.
Alisema kuwa Kitengo cha Kinywa na Meno imefanya ukarabati wa chumba cha kutolea huduma ya kinywa na Meno na kusimika kiti na machine ya X_Ray kwenye vituo cha Afya Ndungu na Hedaru ili kurahisisha utoaji wa huduma.
Kwa upande wake Daftari wa Meno kwenye Hospitali ya Mji-Same Dkt.Taudensia Kilawe amewataka wananchi kuhakikisha kuwa wanapiga mswaki asubuhi na jioni ili kutunza meno.
"Tupunguze pia ulaji wa vitu venye sukari nyingi na kuhakikisha tunapiga mswaki kila tunapotumia vyakula vyenye sukari nyingi"alishauri Dkt Kilawe
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.