Halmashauri ya Wilaya ya Same imeadhimisha siku ya Lishe katika Wilaya hiyo kwa lengo la kuikumbusha Jamii kuzingatia mlo kamili katika kila mlo wanaokula ili kuimarisha afya zao.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni aliwataka wananchi kuzingatia maelekezo ya wataalam wa Lishe ili kuhakikisha kuwa wanaokula mlo ulio bora.
Mkuu wa Wilaya ambaye pia alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonyesho ya vyakula mbalimbali vinavyoimarisha afya aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa kuandaa siku ya lishe ambayo imewawezesha wananchi wengi kupata elimu ya Lishe.
"Hii siku ni muhimu sana kwani inaongeza uelewa wa wananchi kuhusu Lishe bora lakini nichukue nafasi hii kuwahimiza wanawake wajawazito kuhudhuria Clinic ili waweze kupata chanjo mbalimbali lakini pia watoto wote Chini ya miaka mitano wapelekwe clinic ili kujua Maendeleo ya ukuaji wao na pia waweze kupata chanjo" alisema Bi.Kasilda
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi.Anastazia Tutuba aliwataka wazazi wenye watoto mashuleni kuhakikisha kuwa wanachangia chakula ili watoto wao waweze kupata chakula cha mchana shuleni.
Alisema Wilaya ya Same ni miongoni mwa Wilaya zilizosaini Utekelezaji wa Mkataba wa Afua za Lishe ambapo Wanafunzi kupatiwa chakula cha mchana shuleni ni kigezo cha muhimu.
"Tumeshatunga Sheria ndogo ya Mahudhurio ya lazima shuleni na uchangiaji wa chakula shuleni sasa mzazi yeyote asiyetaka kuchangia chakula kwa hiari shuleni basi atakutana na mkono wa Sheria "alisema Bi.Tutuba.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Afisa Lishe wa Wilaya ya Same Bi.Jackline Kilenga amesema kwa sasa Wanafunzi wanaokula shuleni ni asilimia 85 Kati ya Wanafunzi 63,512 wanaopaswa kupata chakula shuleni.
"Kwa upande wa kutembelea Kaya zenye wajawazito na watoto wadogo tumefanikiwa kwa asilimia 100 ambapo Kaya 5,310 zilitembelewa,na Vijiji vyote vina utaratibu wa kuwabana wazazi na walezi juu ya masuala ya Lishe"amesema Bi.Kilenga.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.