Mhe.Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameongozana na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Mbunge wa taifa Mhe.Anne Malechela ,Waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi Mhe.William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Elisha Mngwira.
Akiwa Wilayani Same Mhe.Makamu wa Rais ametembelea na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa shule ya sekondari New Dawn iliyopo kata ya Njoro Mama Samia ameutaka uongozi wa Wilaya ya Same kufanya utaratibu wa haraka kuhakikisha shule hiyo inapata maji na umeme huduma ambazo zitanufaisha na maeneo ya jirani ya shule hiyo.
Baada ya hapo Mhe.Makamu wa Rais alipata fursa ya kuzindua ofisi za wakala wa misitu (TFS) Same na kupanda mti kama ishara ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na TFS katika masuala mazima ya kutunza mazingira ambapo Mama Samiah amewaagiza viongozi wa Wilaya kusimamia na kuhakikisha miti inapandwa maeneo yote ya mjini.
Mkutano wa hadhara ndo ulihitimisha ziara ya Mhe.Makamu wa Rais Wilayani Same. Wakati wa mkutano mama Samia aliongelea mpango wa serikali wa kumshusha mama ndoo kichwani kwa kuleta maji karibu zaidi na makazi ya watu.
Mhe.Makamu wa Rais amezungumzia nia ya serikali ya kuhamasisha na kuwezesha uchumi wa viwanda nchini Tanzania. Amezungumzia maboresho kiwanda cha tangawizi kilichopo kata ya Mamba Miyamba na kuw ataka wahusika waone namna ya kuharakisha matengenezo na kuweka mashine kuanza uzalishaji.
Mhe.Suluhu amewataka wanaSame kuwa na utamaduni wa kupanda miti ili kuleta hali ya hewa nzuri na kutunza mazingira.
Waziri wa ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi amewatoa hofu wanaSame kwamba kero za viwanja na migogoro ya ardhi imekwisha kwani wizara ya ardhi imepewa muda wa miaka mitano na Mheshimiwa Rais kuhakikisha migogoro yote imekwisha.
Aidha Mhe.Lukuvi amewaagiza viongozi wa Wilaya na Halmashauri kuhakikisha mpaka kufikia mwezi desemba 2018 migogoro yote iliyosababishwa na Wilaya na Halmashauri kutatuliwa na kumalizika.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.