Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Mhe.Dr.Anna Elisha Mngwira awafanya wananchi wa kata ya Mtii kuipongeza serikali baada ya kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wa kata hiyo wanaoendelea na ujenzi wa madarasa na kituo cha afya.Akikabidhi mifuko hiyo ya saruji kwa niaba ya mkuu wa mkoa DC wa Same Mhe.Rosemary Senyamule amewapongeza wananchi wa Same kwa hatua ya ujenzi waliyofikia na kuwataka watumie saruji hiyo kwa lengo lililokusudiwa.Pia amemshukuru RC kwa kuchochea ari ya wananchi kufanya msaragambo,na kuwataka wananchi wote kuendelea kuitumia siku ya jumatatu kwa kazi za jamii.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ndugu Isaya Mngulu alipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na CCM kwa kasi kubwa ya maendeleo katika kila nyanja.Awaeleza wananchi miradi mikubwa inayofanywa na serikali.Awachangia fedha kwa ajili ya kupaka rangi jengo la kituo cha afya.
Katika risala yao wananchi waiomba serikali iwasaidie kukamilisha jengo hilo.Na kuwa zinztakiwa kiasi cha fedha shilingi 35 milioni ili kukamilisha jengo zima na wananchi waanze kupata huduma kwani kwa sasa kata nzima hawana huduma za afya.
Waeleza mpango wa "KIJIJI CHANGU FAHARI YANGU" ulivyozaa matunda kwani umewezesha wadau(wacharo) kuchangia na kuanzisha barabara mpya ambayo ni fupi na waiomba serikali kuiingiza kwenye mtandao wa TARURA.Ambapo DC amewahakikishia kuwa itaingizwa.Pia wajitoa kumalizia vyumba 4 kwenye kituo hicho ili huduma za mama na mtoto ziweze kuanza.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.