Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Babu amesema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alifanya kazi kubwa ya kuweka misingi imara ya amani katika nchi yetu hivyo hatuna budi kuendeleza.
Babu aliyasema hayo wakati akifungua Kongamano la siku moja la Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same ambapo alisema watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuilinda amani hii aliyotuachia muasisi wa Taifa letu.
"Leo hii tumekusanyika hapa kusherehekea na kuyakumbuka mema aliyotufanyia baba wa Taifa ni kwasababu tuna amani,bila amani tusiingeweza kukutana hapa,hivyo kila mtu kwa nafasi yake ahakikishe analimda amani ya nchi"alisema Babu
Katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same ikishirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Same mada mbalimbali kuhusu jitihada za Mwalimu Nyerere za kuleta Maendeleo na kupinga ubaguzi ziliwasilishwa.
Mmoja wa watoa mada katika Kongamano hilo,Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki,Jacob Koda ameiomba Serikali kufufua Viwanda vyote vilivyokuwa vikifanya uzalishaji enzi za Mwalimu Nyerere ikiwa kama njia mojawapo ya kumuenzi Mwalimu katika kuinua uchumi.
Askofu Koda aliyasema hayo wakati akitoa mada kuhusu Mchango wa Mwalimu katika kukuza uchumi na Maendeleo endelevu ambapo alisema Nyerere alijitahidi kuanzisha viwanda katika mikoa mbalimbali ili kukuza uchumi.
"Baba wa Taifa alitambua ili nchi iweze kuwa na Maendeleo endelevu lazima kuwe na viwanda na ndipo alipoanzisha viwanda vya nguo kwenye mikoa karibu yote,kulikuwepo pia na viwanda vya ngozi vikitengeneza viatu,mabegi,kulikuwepo na viwanda vya magunia na kiwanda Cha General Tyre cha Arusha ambacho kilikuwa kinaaaminika kwa matairi bora Afrika Mashariki"alisema Askofu Koda.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye alikua mgeni rasmi katika Kongamano hilo aliahidi kuuchukua ushauri huo wa Askofu na kuufanyia kazi.
Kwa Upande wake Profesa Somo Seimu kutoka Chuo Kikuu Cha Ushirika ambaye alitoa mada kuhusu Mchango wa Mwl.Nyerere na dhana ya makundi maalum alisema Nyerere alipinga ubaguzi wa aina zote.
Katika kuhakikisha kwamba makundi yote yanapata utetezi ndipo kulipoundwa Jumuiya mbalimbali ndani ya Chama,Jumuiya hizo ni zile za Wazee,Wanawake na Vijana.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo alisema lengo la kuandaa Kongamano Ni kumuenzi baba wa Taifa lakini pia kuwawezesha vijana kufahamubo mema mazuri aliyoyafanya Baba wa Taifa.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na watu zaidi ya 300 wakiwemo Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro,Madiwani na Watumishi wa Halmashauri ya Same, Viongozi na wanachama wa CCM pamoja na wanafunzi wa Sekondari Wilayani Same.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.