Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Bw.Tixon Nzunda amezindua zoezi la upandaji miti kimkoa kwa kupanda mti katika eneo inapojengwa Hospitali mpya ya Wilaya ya Same.
Baada ya kupanda mti huo Katibu Tawala aliagiza Halmashauri zote kwa kushirikiana na Taasisi binafsi na Taasisi za dini kuhakikisha kuwa wanapanda miti kwa wingi ili kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.
"Tunataka kuwa na Kilimanjaro ya Kijani hivyo kila Taasisi na kila mtu mmojammoja lazima tuhakikishe tunapanda miti ili kulinda Mazingira yetu,leo nimezindua rasmi zoezi hili kwa mwaka huu"amesema Bw.Tixon
Amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Bi.Anastazia Tutuba kuhakikisha kuwa eneo hilo la Hospitali mpya ya Wilaya linakuwa mfano kiwilaya kwa upandaji miti.
Bw.Tixon alisema lengo la Serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro ni kuhakikisha kuwa mabadiliko ya tabia nchi yasiathiri tena Mkoa wa Kilimanjaro na maeneo ya jirani.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi. Anastazia aliahidi kutekeleza maelekezo hayo ya Katibu Tawala.
"Kwa upande wa Halmashauri yetu tunapokea maelekezo yako na tunaendelea kuyafanyia kazi kuhakikisha kuwa Wilaya yetu inakuwa ya Kijani"amesema Anastazia
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kwa mwaka huu Halmashauri hiyo imeshapanda miti zaidi ya 500 na ipo katika hali nzuri,pia amewashukuru wakala wa Misitu (TFS) Kanda ya Kaskazini kwa kuwapatia Miche ya miti kila wanapohitaji.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.