Mkuu wa Wilaya ya Same akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya pamoja na wanawake Wilayani humo wamefanikiwa kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni mbili kwa watoto wenye uhitaji maalum.
Timu hiyo ya wanawake Wilayani Same imefanikiwa kutembelea na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalum wa shule za Msingi Same na Kisima,Kituo cha kulea watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi cha RAFIKI na Mama Mlemavu Mwanaisha Hamisi ambaye ana watoto wawili walemavu.
Akiongoza timu hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe:Kasilda Mgeni alisema misaada hiyo imetolea kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya wanawake ambayo kilele chake ni Machi 8 ya kila mwaka.
Akiwa katika Shule ya Msingi Kisima Mkuu wa Wilaya aliwapongeza waalimu kwa kuweza kuwasimamia na kuwalea vema watoto hao wenye usonji ambao wanahitaji uangalizi wa karibu.
"Kwa namna ya kipekee kabisa niwapongeze walimu kwani naelewa kulea watoto hawa kuna changamoto nyingi lakini mmesimama imara kuhakikisha kuwa wanapata elimu iliyo bora"alisema Mkuu huyo.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anastazia Tutuba amewapongeza wanawake wa Same kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika kuelekea siku ya wanawake duniani Machi 8.
"Ni michango ya wanawake ndio imetuwezesha kuwatembelea watoto na watu wengine wenye uhitaji,wanawake tuendelee kushikamana"alisema Tutuba.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Jasmini Haji aliwashukuru wanawake Wilayani Same kwa msaada waliowapatia.
"Tunashukuru kwa msaada huu na tunaomba Mwenyezi Mungu awaongezee pale walipopunguza"alisema Mwl.Haji
Siku ya wanawake utafanyika kimkoa Wilayani Same,Machi 8 2023 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mhe:Nurdin Babu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.