Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe: Edward Mpogolo amewaagiza mafundi Ujenzi walioshinda zabuni ya ujenzi wa Madarasa kwaajili ya kidato cha kwanza 2023 kuhakikisha kuwa wanakamilisha kazi hiyo kwa muda waliopewa.
Mkuu wa Wilaya alitoa gizo hilo wakati alipoitisha kikao na Wadau wote wa usimamizi wa Ujenzi huo kwa lengo la kuwapa maelekezo muhimu ili kuhakikisha kuwa madarasa hayo yanakamilika kwa wakati.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, wakuu wa Idara na Vitengo,Watendaji Kata,Maafisa Elimu Kata,Wakuu wa shule na Mafundi walioshinda zabuni hizo za ujenzi.
Mkuu huyo alisema Wilaya ya Same imepokea kiasi cha shilingi milioni 640 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 32 kwaajili ya kupokea kidato cha kwanza mwaka 2023 hivyo kila mmoja anapaswa kusimama vema kwenye nafasi yake ili kufikia malengo,
“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa haya madarasa yanakamilika mapema Mwezi Desemba,2022 ili Januari yaweze kupokea wanafunzi,kwahiyo niwasihi mafundi wafanye kila linalowezekana wakabidhi madarasa kwa wakati na fundi anayeona hataweza ajiondoe mapema” alisema Mhe:Mpogolo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mhe:Yusto Mapande amewataka waheshimiwa Madiwani kuhakikisha kuwa wanahamasisha mchango wa nguvu za wananchi katika kusawazisha maeneo ya ujenzi kwani maeneo mengi yana miinuko.
Mhe: Mapande amewataka Wakuu wa shule kusimamia vema ujenzi huo ili ikifika mwezi Januari wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza waingie shule.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Anastazia Tutuba ameahidi kufanya ufuatiliaji wa karibu katika kuhakikisha kuwa madarasa yote yanakamilika kwa wakati uliopangwa.
“Fedha hizi zimegawanywa kwa shule 17 ambazo ndizo zilizokuwa na uhitaji wa madarasa na yatakapokamilika yatatosheleza wanafunzi wanaotarajia kuanza kidato cha kwanza”alisema Tutuba.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.