Halmashauri ya Same imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 62,000,000/= kwa vikundi 18 kwa kipindi cha robo ya nne Aprili-Juni 2019 ambapo vikundi vya wanawake ni 9 waliopata jumla ya shilingi milioni 28,000,000/=,kwa vikundi 7 vya vijana wamepata mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 24,000,000/= na vikundi 2 vya watu wenye ulemavu wamepata mkopo wenye thamani ya shilingi 10,000,000/= ambavyo vimekidhi sifa za kukopeshwa.
Akikabidhi hundi za mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Senyamule ambaye alikuwa ni mgeni rasmi amewapongeza kina mama.vijana na watu wenye ulemavu kwa kupata fursa hiyo ya kupata mkopo ambapo alisema ni agizo la Mhe.John Magufuli kwamba kina mama,vijana na walemavu wapewe mikopo isiyo na riba kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri na kuviasa vikundi hivyo kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi.Mhe.Senyamule amesisitiza vijana kujiepusha na mambo yasiyofaa ikiwemo uvutaji bangi na madawa ya kulevya,kupoteza muda wao mwingi vijiweni bila kazi ,matukio ya ubakaji na uporaji na badala yake waunde vikundi vya kufanya kazi za kimaendeleo.”Vijana ni taifa la kesho,amkeni sasa.”Amesema Mhe.Rosemary Senyamule".
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Same Bi.Anna-Claire Shija amesema Halmashauri inatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi na ahadi ya Mhe.John Pombe Magufuli ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija amewahakikishia wana Same kwamba Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama, vijana na walemavu na kuwataka walengwa hao waunge mkono juhudi hizo kwa kufanya kazi kwa bidii,kulinda mapato ya Halmashauri yasipotee na kurejesha kwa wakati ili zoezi liwe endelevu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.