Halmashauri ya Wilaya ya Same imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 60,000,000/= kwa vikundi 17 ambapo wanawake ni 7,vijana 7 na watu wenye ulemavu 4.Mikopo hii ni kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani shilingi 22,238,000/= na marejesho ya mikopo ya nyuma shilingi 37,864,000/= kwa kipindi cha robo ya tatu 2019/2020 ambapo inakwenda kuwa chachu ya maendeleo ya vikundi,mtu mmoja mmoja na Wilaya kwa ujumla.
Akikabidhi hundi za mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Stack Senyamule ambaye alikuwa ni mgeni rasmi ameipongeza Halmashauri kwa kutoa mikopo hiyo ambapo ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) vilevile amewapongeza kina mama na vijana kwa kupata fursa hiyo ya kupata mkopo ambapo alisema ni agizo la Mhe.John Magufuli kwamba kina mama na vijana wapewe mikopo isiyo na riba kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri na kuviasa vikundi hivyo kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndg.Uledi Lusasi amewahakikishia wana Same kwamba Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama,vijana na walemavu na kuwataka walengwa hao waunge mkono juhudi hizo kwa kufanya kazi kwa bidii,kulinda mapato ya Halmashauri yasipotee na kurejesha kwa wakati ili zoezi liwe endelevu.
Zoezi hilo pia lilihudhuriwa na wadau mbalimbali kama NMB,NSSF na vyama vya ushirika Same Kaya SACCOS.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.