Halmashauri ya Same imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 110,000,000/= kwa vikundi 29 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.Mikopo hii ni kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani kwa kipindi cha robo ya pili 2019/2020 ambapo inakwenda kuwa chachu ya maendeleo ya vikundi,mtu mmoja mmoja na Wilaya kwa ujumla.
Akikabidhi hundi za mikopo hiyo Mkurugenzi Mtendaji Bi.Anna-Claire Shija ambaye alikuwa ni mgeni rasmi amewapongeza kina mama na vijana kwa kupata fursa hiyo ya kupata mkopo ambapo alisema ni agizo la Mhe.John Magufuli kwamba kina mama na vijana wapewe mikopo isiyo na riba kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri na kuviasa vikundi hivyo kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi.Mhe.Mgeni rasmi amesisitiza
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amewahakikishia wana Same kwamba Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama na vijana na kuwataka walengwa hao waunge mkono juhudi hizo kwa kufanya kazi kwa bidii,kulinda mapato ya Halmashauri yasipotee na kurejesha kwa wakati ili zoezi liwe endelevu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.