Ilikuwa ni siku ya furaha na mshangao kwa wawakilishi wa wananchi wakati wa kumkabidhi mkandarasi barabara ya Msanga/Chome.Wananchi wakiri Rais Magufuli ni kiboko.Hawakuwahi kutengenezewa kwa kiwango cha ubora huo tangu Uhuru.
Waoneshwa kazi atakazofanya mkandarasi ili washiriki usimamizi wa fedha za serikali.Watahadharishwa kutoingilia kazi,na wakiona kasoro watoe taarifa TARURA au ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Maeneo korofi kuwekwa zege ili kudhibiti matengenezo ya kila mwaka.
Mradi wagharimu kiasi cha shilingi milioni 700 kwa kilomita 8,mkandarasi CHECOTEC aahidi mradi kukamilika ndani ya miezi mitano.
Naye Mwenyyekiti wa Halmashauri Mhe.Christopher Irira ataka wananchi kuajiriwa na kuwa walinzi wa vifaa.
Meneja TARURA asema fedha hizi zitakuja kwa awamu;na hii ni awamu ya kwanza kwani mahitaji ya kukamilisha barabara nzima ni Tshs.Billion 3.7
Naye DC Mhe.Rosemary Senyamule amesema kukamilika kwa barabara hii kutaifungua fursa kubwa ya utalii iliyopo kata ya Chome,kwani ndipo ilipo njia ya kufika kilele cha mlima Shengena ambacho ni cha pili kwa urefu kwa mkoa wa Kilimanjaro.Pia itarahisisha usafirishaji wa abiria,wagonjwa na mazao.
Ziara hiyo iliwahusisha TARURA,Mkandarasi,DC,DED,Mwenyekiti wa Halmashauri,viongozi wa kata na vijiji ambao walitembelea kwa mguu eneo kubwa ili kuona kazi inayotegemewa kufanyika.
Hakika Ilani ya CCM inatekelezwa.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.