Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Edward Mpogolo leo tarehe 01/09/2021 ameongoza zoezi la kugawa pikipiki kwa watendaji wa kata 15 zilizopo wilayani Same ambapo pikipiki hizo zimenunuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa lengo la kutumika katika shughuli za kukusanya mapato na miradi ya maendeleo.
Mhe.Mpogolo ameipongeza Halmashauri kwa kazi kubwa ambayo imeendelea kufanya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutumia fedha ya Serikali vizuri kwa kununua pikipiki 16 ambapo pikipiki 15 zimegawiwa kwa watendaji wa kata 15 na pikipiki 1 wamepatiwa kitengo cha biashara na mapato Halmashauri kwa ajili ya shughuli za mapato na guta 1 wamepatiwa mamlaka ya mji mdogo wa Same kwa ajili ya shughuli za usafi.
Mhe.Mpogolo amewaagiza watendaji wa kata waliopata pikipiki kutuzitumia kwa lengo lililokusudiwa ili kuongeza mapato ya Halmashauri.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Yusto Mapande amewaasa watendaji kwamba pikipiki hizo zitumike katika shughuli za kukusanya mapato na usafiri kwa kata zisizo na usafiri.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.