Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama ameshauri wananchi kushiriki kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.
Ameyasema hayo wakati akikabidhi mipira 130 kwa baadhi ya walimu wa Michezo kutoka Shule za Msingi na Sekondari Wilayani Same ili kuimarisha Michezo mashuleni.
Mipira hiyo ilikabidhiwa Wilaya ya Same na Shirikisho la Mpira Wa Miguu nchini (TFF) Kwa lengo la kuimarisha Michezo na kuibua vipaji mashuleni.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Afisa Michezo na Utamaduni Wilaya ya Same Bw.Nevlin Nyange ameishukuru TFF kwa msaada huo na kuahidi kutumia vema mipira hiyo katika kukuza vipaji.
"Tunashukuru sana TFF kwa msaada huu na tunaahidi kwamba tutaitumia vema kuhakikisha kwamba tunashinda mashindano ya UMISETA NA UMITASHUMTA"Alisema Nyange.
Nae Mratibu wa UMITASHUMTA Wilayani Same Mwl.Nathaniel Msangi aliwataka walimu wa michezo kushirikiana na jamii kwenye maeneo yao katika kuibua na kukuza vipaji.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.