Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Elisha Mnghwira amezindua kituo cha kuuzia madini cha mkoa wa Kilimanjaro kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Same ambapo ni agizo la Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli kwamba kila Mkoa uanzishe kituo cha kuuzia madini.Kituo cha kuuzia madini kimezinduliwa Wilayani Same kwa kuwa ni wilaya inayoongoza kuwa na madini mengi zaidi kuliko wilaya nyingine za mkoa wa Kilimanjaro kama Moshi Vijijini,Mwanga,Rombo na Siha.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali kama TAWOMA,KILEMA,Wafanyabiashara wa madini mkoa wa Kilimanjaro,wachimbaji wa madini,Taasisi za kifedha ambazo ni NMB,CRDB,NBC,TPB na TRA.
Mhe.Anna Mnghwira amesema kituo cha kuuzia madini kimezinduliwa ili kuwa na sehemu maalumu ya kuuzia madini na kuwapa urahisi wafanyabiashara wa madini kufanya biashara hiyo kwa uhalali ili kukuza uchumi wa nchi na kufwata sheria.Mhe.Mnghwira amewaasa wana Kilimanjaro kuwapa kipaumbele wanawake kwamba wanaweza na amewataka kina baba kuwawezesha kina mama kuwa na uchumi mzuri kwa kuwa mwanamke ni mkombozi wa jamii katika nyanja zote.
Vilevile Mhe.Mnghwira amewataka wachimbaji wa madini kuyafikisha madini kwenye kituo cha kuuzia madini bila kuchakachua.
Mhe.Mkuu wa Mkoa ameziagiza Taasisi za fedha kutoa mikopo itakayoweza kuwasaidia wachimbaji na kwa kuzingatia muda wa kuanza kurejesha mikopo hiyo.Vilevile TRA waagizwa kutochukua mapato mpaka kwenye mizizi ili wafanyabiashara waweze kupata faida.
Aidha Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi waagizwa kusimamia sheria na taratibu ili kuhakikisha kwamba madini yanayotolewa machimboni yanafikishwa katika kituo cha kuuzia madini yakiwa na ubora na uhalisia uleule.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.