Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro Jonathan Mabihya amewataka wananchi Wilayani Same kuhakikisha wanalinda miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali Wilayani humo.
Mabihya alitoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kalemawe alipotembelea kukagua ujenzi wa daraja la mawe Kalemawe lililojengwa kwa gharama ya Shilingi milioni 376.
Katibu huyo ambaye alikiwa ameongozana na Kamati ya Siasa ya Mkoa na wamefanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM (2020-2025).
"Serikali inatumia fedha nyingi Sana kutekeleza Miradi ya Maendeleo na lengo ni kuondoa kero kwa wananchi hivyo hakikisheni mnatunza Miradi hii"alisema Mabihya.
Akitoa taarifa ya Ujenzi wa daraja la mawe Meneja wa TARURA Wilaya ya Same Mhandisi James Mnene alisema daraja hilo limejengwa kwa Tsh.mil 376 na limekamilika kwa asilimia 98.
"Daraja hilo lina urefu wa mita 36 na upana wa mita tisa na lina uwezo wa kubeba tani 37 bila wasiwasi pia umri wake wa kutumika ni miaka 100"alisema Mnene.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anastazia Tutuba amesema Ujenzi huo unachangia ongezeko la mapato ya Halmashauri ambapo wafanyabiashara hupata urahisi wa kusafirisha mazao na hivyo kuchangia mapato ya Halmashauri.
Kwa upande wake Mwananchi wa eneo hilo Amina Gadi aliishukuru Serikali kwa kuwajengea daraja hilo kwani limekua msaada mkubwa kwao.
"Tunaishukuru Sana Serikali kwa kutujengea hili daraja ambalo limekuwa msaada mkubwa kwetu,wanafunzi wanavuka kirahisi kwenda shule na wakulima tunasafirisha mazao kirahisi"alisema Amina.
Katika Ziara hiyo Kamati ya siasa ilitembelea Miradi ujenzi wa daraja la mawe,ujenzi wa eneo korofi barabara ya Hedaru-Vunta-Myamba,ujenzi wa Barabara ya Maore-Mpirani-Ndungu.
Miradi mingine iliyotembelewa ni Mradi wa maji Mabilioni -Hedaru,ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na Ukarabati wa mabweni mawili shule ya Sekondari Same.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.