Ni utalii katika msitu wa Chome kilele cha Sheghena ambapo wilaya ya Same imedhamiria kutangaza kivutio hiki ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea. Dc Same aliongoza jopo la wataalamu 23 kutoka ofisi za serikali wilayani hapo wakiratibiwa na TFS kupanda mlima mrefu wa 2462Mt. Toka usawa wa bahari, kilele cha pili kwa urefu kufuatia mlima kilimanjaro kwa mkoa.
Vivutio vya miti, ndege, vipepeo, nyani, mito na uoto wa asili ni rasilimali kubwa. Ni eneo unaloona mlima kilimanjaro kwa juu zaidi kuliko eneo jingine linafaa kwa utalii, mazoezi ya kupanda mlima kilimanjaro, kurekodi sinema, hifadhi ya mazingira, uwekezaji, utafiti, vyanzo vya maji, campsite. TFS wafikiri kuweka skyline.
"Ni lazima tujipange kufanya vitu vya tofauti ili kuwafanya watalii kuchagua sheghena" alisema DC Same. Pia aliwaalika watu kuja kujionea uumbaji wa Mungu uliopo sheghena.
Aidha Mhe. Rosemary Stacki alitoa tahadhari kwa wenye nia ya kuchezea msitu huo kwa kuwa ni moja ya Wilaya ya Same kwani vyanzo vya maji zaidi ya 8 vinavyotegemewa na wananchi vinaanzia msitu huo. Aahidi kuutunza, kuulinda na kuuthamini na kuwachukulia hatua wanaochezea Mlima Sheghena.
Timu hiyo ilitumia kati ya saa 2:30 - 2:40 kufika kileleni umbali wa kilomita 5.54.
\
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.