Ni maneno yaliyosemwa na wananchi wa kijiji cha Mhezi walioamua kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa shimo la kutupa kondo la nyuma na jengo la kuchomea taka katika zahanati ya Mheza.DC wa Same Mhe.Rosemary Senyamule aliyeamua kushirikiana na wananchi wa wilaya yake kila jumatatu kwa kufanya kazi za kijamii,alishiriki kazi hiyo ya kusomba mawe kwa kiwango sawa na wananchi wengine.
"Kama tulitumia nguvu zetu nyingi kufanya kazi kwa faida ya wengine utumwani,hebu sasa tutumie nguvu ile ile kufanya kazi kwa maendeleo yetu.Hakika tutaona maendeleo ya haraka Same"Alisema DC huyo.Aliwaasa viongozi wa kijiji na kata kushirikiana na wananchi kwa kufanya nao kazi na sio kuwasimamia kwa kusema,uongozi ni vitendo na sio maneno.
Baada ya kazi hiyo DC pamoja na wataalam alioongozana nao walitumia nafasi hiyo kusikiliza kero za wananchi wa Mhezi na kuzitolea majibu.
Wananchi wa Mhezi walipongeza serikali ya awamu ya tano na Mhe.Rais John Pombe Magufuli kwa kupata huduma ya maji maeneo mengi pamoja na mradi tarajiwa,pia waliomba kupata umeme maeneo yaliyobaki.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.