Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Godfrey Mnzava ameagiza Wizara ya Maji kuhakikisha kuwa Mradi mkubwa wa Maji wa wa Same-Mwanga-Korogwe (SMK) unakamilika ifikapo mwezi Juni 2024 kama alivyoagiza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Philip Mpango.
Kiongozi huyo alitoa agizo kufuatia maombi ya Mbunge wa Same Magharibi Mhe.David Mathayo ambaye aliwakilisha changamoto ya upatikanaji wa Maji ya uhakika kwa wakazi wa Same.
"Tunashukuru tangu alipofika Makamu wa Rais Mhe.Philip Mpango tumechimbiwa visima kadhaa ambavyo vimesaidia kwa kiasi kupunguza changamoto ya Maji,lakini bado tunahitaji Maji ya kutosha"alisema Dkt Mathayo.
Kufuatia maombi hayo Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2024 Ndg Mnzava aliagiza Mradi mkubwa wa Maji wa SMK kukamilika mwezi Juni 2024 kama alivyoagiza Makamu wa Rais Mhe.Philip Mpango.
Mwenge wa Uhuru umewasili Wilayani Same April 8 na umeweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Barabara Km 1.4 za kiwango cha lami nyepesi ambayo imegharimu shilingi milioni 980.9.
Mwenge wa Uhuru umetembelea Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Mother Kevina kilichopo Kata ya Kisima ambacho kinalea watoto 44 wakiwemo watoto wadogo wa Shule za Msingi, Sekondari na wa vyuo.
Kwenye Kituo cha Mother Kevina Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Ndg.Mnzava amekabidhi hundi ya shilingi milioni tatu fedha zilizotokana na michango ya Mwenge kwaajili ya kuwezesha ununuzi wa viti mwendo viwili.
Mwenge wa Uhuru umetembelea pia Kikundi cha Wajasiriamali cha Wandeme ambacho kinajishughulisha na kutengeneza samani za majumbani na za Ofisini.
Kikundi hicho kina mtaji wa milioni 10 na kilipatiwa mkopo wa milioni mbili kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Same.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni ameitaja Miradi mingine itakayofikiwa na Mwenge wa Uhuru 2024 kuwa ni Mradi wa Kitalu cha Miti Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ambao umegharimu Shilingi milioni 79.
Mwenge wa Uhuru 2024 umezindua pia Klabu ya Wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Makanya.
Ukiwa Wilayani Same Mwenge wa Uhuru umezindua Mradi wa Maji wa Kijomu- Mabilioni ambao umegharimu shilingi milioni 447.7
Mradi wa Maji Kijomu-Mabilioni umesaidia kuondoa Kero ya upatikanaji Maji kwa zaidi ya wananchi 2,000
Mwenge wa Uhuru utazindua jengo la mama na Mtoto kwenye Kituo cha Afya Hedaru,jengo ambalo Ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 528 ambapo milioni 8 kati ya fedha hizo zinatokana na nguvu za wananchi.
Katika Wilaya ya Same Mwenge wa Uhuru umefikia Miradi nane yenye thamani ya Tsh.Bil.3.6
Baada ya kukamilisha ziara yake Wilayani Same,Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa Mkoani Tanga April 9 katika eneo la Mazinde.
Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.