Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2023 Ndg. Abdallah Shaib Kaim ameeleza kuridhishwa na Ubora wa Miradi saba ya Maendeleo aliyoitembelea katika Wilaya ya Same wakati Mwenge wa Uhuru ulipokimbizwa Wilayani humo.
Mwenge wa Uhuru uliwasili na kukimbizwa katika Wilaya ya Same Juni 20 mwaka huu ambapo Mwenge huo ulifikia Miradi saba ikiwemo Miradi ya Afya,Maji,Elimu,Mazingira, Barabara na Ujasiriamali yenye thamani ya shilingi Bil.3.68.
Akizungumza baada ya kukagua Miradi hiyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg.Abdallah alisema ameridhishwa sana na Ubora wa Miradi na mpangilio mzuri wa Nyaraka za Miradi yote iliyofikiwa na Mbio za Mwenge.
“Tumefanya Ukaguzi wa kina wa Miradi na Nyaraka,tumejiridhisha na Ubora na thamani ya fedha,niwapongeze sana Mkuu wa Wilaya,Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi kwa usimamizi makini wa Miradi” alisema Ndg.Abdallah
Awali akipokea Mwenge wa Uhuru Mkoani Kilimanjaro ukitokea Mkoa wa Tanga, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw.Nurdin Babu alisema ukiwa Mkoani Kilimanjaro Mwenge wa Uhuru utafikia Miradi 45 yenye thamani ya shilingi Bil.30.3 na ulianzwa kukimbizwa katika Wilaya ya Same.
Baada ya Mkuu wa Mkoa kupokea Mwenge wa Uhuru aliukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mshikizi Bw.Amir Mkalipa kwaajili ya kuanza kuukimbiza katika Wilaya ya Same.
“Katika Wilaya ya Same tutakimbiza Mwenge wa Uhuru kwenye umbali wa Kilomita 102 na utafikia Miradi ya Maendeleo saba yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.86”alisema Bw.Amir
Ukiwa Wilayani Same Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa kona korofi za barabara ya Hedaru-Vunta –Myamba(mita 810)wenye thamani ya shilingi milioni 655.5.
Mwenge pia ulizindua Madarasa Mawili katika shule ya Sekondari Chauka yenye yaliyojengwa kwa thamani ya shilingi mil.42.6 ambazo ni mgawo wa fedha za tozo,katika shule ya Chauka Mwenge Ulizindua pia Klabu ya Wapinga Rushwa.
Mwenge pia uliweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Zahanati ya Saweni ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 95,Mwenge pia ulitembelea Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Wilaya ya Same ambayo katika awamu ya kwanza ujenzi wake umegharimu Shilingi bilioni 2.
Miradi mingine iliyofikiwa na Mwenge Wilayani Same ni Mradi wa Maji Mwembe wenye thamani ya shilingi 662.1 ambao ulizinduliwa pia Mwenge ulizindua Kitalu cha Miti TFS chenye thamani ya shilingi Mil.112.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.