Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Mhe.Anna Mnghwira ashiriki katika kikao maalumu cha baraza la hoja ambapo hoja za miaka ya nyuma idadi ni 63,hoja zilizofungwa ni 40.hoja zilizobaki ni 23 ambapo hoja zilizobaki zimeshatafutiwa majibu na kuwasilishwa ofisi ya mkaguzi mkuu wa mkoa tayari kwa ajili ya uhakiki.
Hoja za mwaka ulioishia tarehe 30 juni 2018 idadi ni 49,hakuna hoja zilizofungwa,hoja zilizobaki ni 72 ambapo majibu ya hoja zilizobaki yameshawasilishwa kwa Mkaguzi Mkuu wa nje (chief External Auditor) kwa ajili ya kuzifanyia uhakiki na kuzifunga.
Hoja za mradi wa maji miaka ya nyuma idadi ni 7,hoja zilizofungwa ni 2,hoja zilizobaki ni 5 ambapo hoja zilizobaki zimepatiwa majibu na nyaraka husika zimewasilishwa kwa mkaguzi wa nje kwa ajili ya uhakiki na kwa mwaka 2017/2018 idadi ni 9,hoja zilizofungwa hakuna,hoja zilizobaki ni 9 jumla ni hoja 14 ambapo hoja zilizobaki zimepatiwa majibu na nyaraka husika zimewasilishwa kwa mkaguzi wa nje kwa ajili ya uhakiki.
Hoja za mradi wa mfuko wa pamoja wa afya kwa miaka ya nyuma idadi ni 15,hoja zilizofungwa ni 7,hoja zilizobaki ni 8 ambapo hoja zilizobaki zimeshatafutiwa majibu na kuwasilishwa kwa mkaguzi mkuu(Chief External Auditor) kwa uhakiki.Hoja za mwaka 2017/2018 idadi ni 7,hoja zilizofungwa hakuna,hoja zilizobaki ni 7 jumla ni hoja 15 ambapo hoja zilizobaki zimeshatafutiwa majibu na kuwasilishwa kwa mkaguzi mkuu(Chief External Auditor) tayari kwa ajili ya uhakiki.
Naye Mkuu wa Mkoa Mhe.Anna Mnghwira ameagiza uongozi wa Halmashauri kupunguza hoja za mapungufu na kuchelewa miradi.Mhe.Mkuu wa Mkoa apongeza kutokuonekana kwa mifuko ya plastiki na amewataka watu wa misitu na mazingira kukaa pamoja ili kupangilia vichaka vilivyopo pembezoni mwa barabara.
Mhe.Anna Mnghwira amechangia mifuko mia moja (100) ya saruji katika shule ya msingi Igulunde iliyopo kata ya Mtii wilayani Same ambapo ni hoja iliyoibuliwa na Diwani wa kata hiyo Mhe.Heriel Msolo kwamba ni muda mrefu mradi wa shule hiyo haukamiliki.
Picha hapo juu ikimuonesha Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Christopher Irira akiongea katika kikao cha baraza maalum cha hoja
Picha hapo juu ikimuonesha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Same Bi.Anna-Claire Shija akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri afungue kikao maalum cha baraza la hoja.
Picha hapo juu ikiwaonesha Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Same wakiwa katika kikao maalum cha baraza la hoja.
Picha hapo juu ikiwaonesha wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa katika kikao maalum cha baraza la hoja.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.