Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Senyamule ameungana na maamuzi ya kikao cha baraza maalum la madiwani wa Halmashauri ya Same cha tarehe 26/27 mwezi Februari 2019 kilichopitisha bajeti ya shilingi 47,765,787,914.00 kwa mwaka wa fedha 2019/20.
Katika bajeti hiyo shilingi 39,391,572,281.74 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi,shilingi 1,670,891,000.00 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo(Ruzuku) na shilingi 2,551,621,430.00 ni kwa ajili ya mapato ya ndani.Pamoja na hayo shilingi 3,189,789,500.00 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa baraza hilo maalum leo tarehe 27.02.201 Mhe.Senyamule amewataka watumishi wa Wilaya ya Same kuwajibika ipasavyo kila mmoja kwa nafasi yake ili kufikia malengo ya mafanikio kiwilaya sambamba na kauli mbiu ya Mhe.Raisi John P.Magufuli ya “hapa kazi tu”
Wakati huohuo amesisitiza wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuchangia masuala ya kimaendeleo ikiwemo miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Wilaya ya Same.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Irira ametoa wito kwa wanasiasa wanaokataza wananchi kuchangia shughuli za kimaendeleo ikiwemo miradi mbalimbali ya kijamii na ukusanyaji wa mapato ya ndani,Mhe.Irira ameongeza kwamba wao (wanasiasa) ndio chachu ya maendeleo katika maeneo yao na lengo la pamoja ni kuhakikisha watu wa Same wanapata maendeleo kwa wakati katika Nyanja zote bila kujali itikadi ya vyama vyao.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.