Ni siku ya uzinduzi wa kamati ya lishe wilayani Same ni agizo na kipaumbele cha serikali ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Same Mhe.Rosemary Senyamule ambaye alizindua kamati hiyo ya lishe ya wilaya Mwenyekiti wa kamati hiyo akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija,katibu ni mganga mkuu Dr.Godfrey Andrew na wajumbe wengine ni wakuu wa idara na vitengo mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Same na wajumbe wengine ni viongozi wa dini na mashirika mbalimbali kama muongozo unavyoelekeza.
Akizindua kamati hiyo Mhe.Senyamule amesema kama kamati ya lishe ya wilaya kuna kazi kubwa ya kufanya kwa maswala yanayohusiana na lishe ambapo ametoa madhara ya kuwa na lishe duni na faida za kuwa na lishe bora kwamba humwezesha mtu kufanya kazi kwa bidii na kutekeleza vyema majukumu yake na kwa watoto humsaidia kufanya vizuri katika masomo yake.Mhe.Senyamule aliwapongeza waliochaguliwa kuwa wanakamati na kuwataka wawajibike katika majukumu yao kama kamati."Lishe bora ni msingi wa maendeleo yetu kwa ujumla"alisema Mhe.DC.
Naye mganga mkuu Dr.Godfrey Andrew alitoa taarifa fupi juu ya hali ya lishe wilaya ya Same na utekelezaji wa viashiria vya lishe wilaya ya Same,hali halisi ya utekelezaji katika kipindi cha mwaka 2017-2018 ikiwemo fedha zilizotengwa katika utekelezaji wa masualaya lishe katika Halmashauri,bajeti ya wadau na uboreshaji wa huduma za lishe nchini,vikao vya kamati za lishe vya halmashauri,usimamizi shirikishi wa shughuli za lishe,kiwango cha utoaji wa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu(FEFO),kutoa huduma ya nyongeza ya matone ya vitamin A kwa watoto walio na umri wa miezi 6-59 na changamoto ambapo changamoto mojawapo ni uhaba wa watoa huduma wa ngazi ya jamii waliopewa mafunzo juu ya unahisi na elimu za lishe ngazi ya jamii.
Afisa lishe wa Wilaya Bi.Jackline Kileng'a akiwasomea wajumbe wa kamati majukumu yao kama muongozo unavyoelekeza.
Naye mwenyekiti wa kamati ya maafa wilaya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija aliwashukuru wanakamati na kufunga kikao ambapo aliwataka wanakamati kutekeleza majukumu yao kutokana na nafasi zao.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.