Mkuu wa Wilaya Mhe. Rosemary Senyamule aliyekuwa mgeni Rasmi kwenye shughuli hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro azinduzia Harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa iliyofanyika Wilayani Same tarehe 05/04/2018.Ahadi za vifaa zatolewa kama saruji tani 25, mabati na mbao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same atoa ahadi ya tani moja ya mifuko ya saruji,Mbunge wa Same Mashariki Mhe.David Mathayo atoa ahadi ya shilingi milioni kumi(10),Mhe.Anna Kilango atoa ahadi ya shilingi milioni sita(6) na Mhe.Angela Kairuki atoa ahadi ya shilingi milioni tano(5).Wananchi wa Same na mashirika binafsi waongoza kwa uchangiaji.
Madarasa 50 kujengwa kwa kushirikisha nguvu za wananchi,Kata zitakazoandaa mawe na matofali ndizo zitaanza kupewa.Hamasa yatolewa wengine kuendelea kuchangia kwani upungufu wa madarasa bado ni mkubwa.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Rosemary Senyamule aliyekuwa mgeni Rasmi kwenye shughuli hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro awashukuru na kuwapongeza wote waliofanya kazi hiyo nzuri.Aagiza waliotoa ahadi kumaliza kabla ya tar. 30 Mei, 2018 kwani tar. 01 Juni, 2018 kutakuwa na uzinduzi wa ujenzi huo. Aagiza halmashauri kuandaa mpango mzuri wa matumizi na usimamizi ili kupunguza tatizo la madarasa." Shukrani nzuri ya kuwapa hawa waliotuchangia leo ni kufanya vizuri kwenye elimu" Alisema Mkuu huyo wa Wilaya. Awataka wanafunzi, wazazi, walimu, kushiriki kuongeza ufaulu ili kuendelea kuwatia moyo wadau kwani bado kuna mahitaji mengi kwenye elimu. Akemea wanasiasa wanaopinga maendeleo, ataka wachukuliwe hatua.Awashukuru wabunge na madiwani wa CCM kwani ndio walioshiriki. Wafanyabiashara, mashirika SUMATRA, PPF, GEPF, TANAPA, EWURA, TFS, Taasisi za dini, Mashirika yasiyo ya kiserikali.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.