Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghwira aliyekuwa mgeni rasmi siku ya sherehe ya wauguzi mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika wilayani Same amewaagiza wauguzi kutimiza wajibu wao ili wasiingiliwe,kwani wasipotimiza wajibu ni lazima wataingiliwa.Aagiza halmashauri ambazo hazijawapa sare kufanya hivyo.Awapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na kutaka watu wote tuwatie moyo kwani ni kazi ya wito.
Naye Mkurugenzi wa wauguzi Tanzania toka Wizara ya Afya Ndg.Moyo aliyehudhuria sherehe hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu alitoa salamu za Wizara na kutoa ufafanuzi wa maombi yaliyojitokeza kwenye risala ya wauguzi,awataka wauguzi kuweka maazimio wanayotaka kuyafikia kila mwaka wanapokula kiapo.
Yaelezwa wauguzi wanaweza kuokoa vifo vya mama na mtoto kwa asilimia 70% bila msaada mwingine.Sherehe iliadhimishwa kwa kutoa huduma kwa jamii kwa kupima sukari,BP,HIV na huduma ya kutoa damu ambapo chupa 30 zilipatikana.
Siku hii huadhimisha Tar.12 Mei ya kila mwaka kumkumbuka muasisi wa wauguzi duniani Ndg.Florance Nightngare.Zawadi zilitolewa kwa wauguzi bora.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.