Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija akiwa ameambatana na wataalamu kutoka idara na vitengo mbalimbali azungumza na wananchi wa kata ya Same mjini juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo,mapato na matumizi.
Moja ya miradi aliyoizungumzia ni mradi wa maji toka Nyumba ya Mungu,mradi wa kituo cha afya Ndungu,Shengena na Kisiwani.
Katika mradi wa maji kutoka Nyumba ya Mungu Bi.Anna-Claire Shija alisema mitaro na visima ipo tayari na hivi karibuni Same itapata maji kutoka Nyumba ya Mungu,kwa upande wa vituo vya afya Bi.Anna-Claire Shija amesema serikali imetoa jumla ya bilioni 1.2 na kituo cha Ndungu na Shengena vipo kwenye hatua za mwisho za ukamilishwaji ili vianze kutumika.
Wananchi wa kata ya Same mjini watoa kero mbalimbali zikiwemo za maji,migogoro ya ardhi na barabara.Wataalamu wa maji,afya,ardhi,TARURA wajibu kero hizo.
Aidha,Bi.Anna-Claire Shija asisitiza wananchi wa Same kujiunga na CHF iliyoboreshwa ili kupata huduma za afya pindi wanapougua,amesisitiza pia wananchi kulipa kodi kwa hiari ili serikali ipate mapato,wanawake na vijana kujiunga kwenye vikundi halali vya ujasiriamali ili wapewe mikopo,usafi wa mazingira kwa ujumla vilevile Bi.Shija awaasa watunishi wa idara ya afya kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa hasa kwa wamama wajawazito.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.