Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija ametembelea mgodi wa madini ya Magnesite uliopo kata ya Mwembe ambapo ameongea na vibarua na wafanyakazi mgodini hapo ili kujua kama halmashauri inapata mapato sawa na wanachokichimba na utaratibu mzima wa jinsi ya kukusanya mapato hayo.
Madini hayo ya magnesite yanasafirishwa kwenda mkoa wa Tanga na hutumika kutengenezea tiles,kwa lori moja ushuru unaotozwa ni Tshs 45,000/= ambapo ni mapato ya Halmashauri..
Bi.Shija asikiliza changamoto mbalimbali za vibarua hao,atoa ushauri na kuahidi kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto hizo.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.