Wafugaji Wilayani Same wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatekeleza agizo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi la uwekaji hereni za utambulisho na usajili wa kielekroniki kwa mifugo kabla ya tarehe 31 Oktoba 2022 .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Anastazia Tutuba amesema baada ya tarehe 31 Oktoba 2022 hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wafugaji ambao mifugo yao haijawekwa hereni za kieletroniki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini au kifungo.
Alisema adhabu nyingine Ni pamoja na mifugo isiyokuwa na hereni kutoruhusiwa kuuzwa minadani,machinjioni pia kuzuiliwa kibali cha kusafirishwa.
"Zoezi la uwekaji hereni za kielekroniki kwa mifugo linasaidia kutambulika kwa mifugo na maeneo mifugo hiyo inakotoka,kupatauhakika wa soko la mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi"Alisema Tutuba.
Amezitaja faida nyingine kuwa Ni kuwezesha Serikali na Wadau kuweka mipango madhubuti ya kuboresha huduma za mifugo, Kudhibiti wizi wa mifugo,kusaidia kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ya mifugo.
Akizungumzia Maendeleo ya zoezi hilo Wilayani Same,Afisa Mifugo Dk.Cainan Luponelo amesema muitikio ni mzuri na zoezi linaendelea katika Kata zote zenye mifugo.
"Ni siku kumi zimepita tangu tuamze zoezi hili kwenye Wilaya yetu lakini tayari mifugo 2,905 imeshasajiliwa kwa kuvalishwa hereni za kielektronik"alisema Dk.Cainan
Aliitaja mifugo iliyovalishwa hereni hizo kuwa ni Ng'ombe 1,243,Mbuzi 1,025,Kondoo 582 na Punda 55 ambapo alisema zoezi hilo linaendelea.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.