Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni amemuonya mwekezaji wa shamba la Mkonge la LM Investment kuacha kutoa taarifa mitandaoni kwamba wananchi wamevamia na kuchoma moto eneo lake wakati sio kweli.
Mkuu wa Wilaya ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Ndungu na Maore ambazo zinapakana na shamba hilo ambapo alisema taarifa za mwekezaji huo zinazorushwa mitandaoni zinazua taharuki.
“Nimetembelea eneo linalolalamikiwa na nimekagua maeneo yote ya shamba hilo yanayopakana na wananchi lakini eneo pekee nililokuta limechomwa na kusafishwa ni eneo panapojengwa shule ya Sekondari” alisema Mkuu huyo.
Mkuu wa Wilaya alimtaka Mwekezaji huyo kuacha kuzua taharuki mitandaoni kwani eneo lake lipo salama na hakuna mtu aliyevamia eneo lake kwani eneo linalosafishwa ni mali ya Kijiji cha Misufini.
Mapema mwezi Agosti mwaka huu Serikali ilipunguza ekari 300 kutoka katika shamba la LM investment na kuzigawa kwa vijiji vya Mpirani,Misufini na Ndungu ambapo kila kijiji kilipata ekari 100.
Akizungumza katika Mkutano huo Diwani wa Kata ya Maore Bw.Issa Rashid alimueleza Mkuu wa Wilaya kuwa hakuna mwananchi yeyote aliyevamia eneo la mwekezaji.
“Huyu mwekezaji yupo hapa miaka mingi sana na hata kipindi kile tunahangaika tugaiwe maeneo kwaajili ya wananchi wetu tulikuwa wavumilivu zaidi ya miaka kumi hadi tukagaiwa eneo letu sasa leo tumeshapewa eneo ndo tuje tufany fujo” alihoji diwani huyo.
Diwani huyo alimuahidi Mkuu wa Wilaya kwamba Wananchi wake hawatafanya fujo yoyote wala hawawezi kuvamia eneo la Mwekezaji ila wanachosubiri wao ni kupatiwa hati miliki za maeneo waliyopewa.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.