Mkuu wa Wilaya ya Same,Mhe Kasilda Mgeni amekabidhi pikipiki sita zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa Watendaji Kata wilayani Same.
Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka watendaji kutumia pikipiki hiyo kwa malengo tarajiwa ya kuboresha utoaji wa huduma na ukusanyaji wa mapato ya serikali.
"Serikali imewathamini na kuwapatia Vitendea kazi,hivyo ni vyema pikipiki hizo zikatunzwa na kutumika kwa malengo tarajiwa"alisema Mhe:Mgeni.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Anastazia Tutuba ameishukuru Ofisi ya Rais Tamisemi kwa Msaada huo ambao amesema utasaidia kuboresha utendaji kazi.
Naishukuru Sana Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kutupatia pikipiki hizi ambazo tuna imani kubwa kuwa zitasaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato.
"Kwa mwaka Jana Halmashauri yetu ilifanikiwa kununua pikipiki 16 za watendaji wa Kata,hivyo tayari Kata 22 Kati ya 34 zina pikipiki,lengo ni kuhakikisha kata zote zinapata pikipiki"alisema Tutuba
Nae Mtendaji Kata wa Mshewa, Benedict Lopa ameishukuru serikali kwa kuwapatia Vitendea kazi na kuahidi kutumia kwa malengo tarajiwa.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.