Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Kasilda Mgeni amezindua kampeni maalum ya kuotesha miti kwenye Wilaya ya Same ili kutunza mazingira na kuvutia Utalii.
Akizungumza katika Uzinduzi huo Mhe.Kasilda amesema zoezi hilo linaanzia kwenye Taasisi za Serikali zikiwemo Hospitali,vituo vya Afya na Shule.
Zoezi hilo ni utangulizi wa Tamasha la Utalii Same (Same Utalii Festival) linalotarajia kufanyika Wilayani Same mwezi Desemba Mwaka huu.
"Tunapozungumzia Utalii,tunazungimzia wanyama ambao wanahitaji mazingira mazuri ili waweze kustawi na kuendelea kuwepo,hivyo tunaotesha miti ili kustawisha uwepo wa wanyama ambao ndio wanaovutia Utalii"amesema Mhe Kasilda
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wa Wilaya ya Same kuunga mkono juhudi za Serikali za kutunza mazingira kwa kila kaya kuotesha miti mitano.
Mkuu wa Wilaya pia aliishukuru Kampuni ya Tanzania Footmark Safari kwa kuchangia miti laki moja ili kufanikisha zoezi hiyo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anastazia Tutuba amesema lengo la Halmashauri ni kuhakikisha kuwa Wilaya inafikia lengo la kuotesha miti mil 1.5 kila mwaka.
"Tumeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa miti yote inayooteshwa inastawi na tunazo Sheria ndogo za kuhakikisha wale wote wanaolisha mifugo katika maeneo yaliyooteshwa miti wanachukuliwa hatua maana mifugo ndio inayoharibu miti yetu"amesema Bi.Tutuba.
Mkurugenzi huyo ametoa shukrani kwa Taasisi na mashirika yanayowezesha miche ya miti Wilayani humo wakiwemo Wakala wa Misitu nchini (TFS),shirika la FLORESTA na Same NG'Os platform.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.