Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Senyamule katika ziara zake vijijini alikutana na kero kuwa watumishi wote wa kata hiyo hawakai katika eneo la kazi na hivyo wananchi kukosa msaada wanapohitaji huduma za haraka.
Aagiza kabla ya tarehe 30/09/2019 watumishi wote wawe wamehamia kwenye maeneo yao ya kazi.Awasifu wananchi wa Same kwa kujenga nyumba bora ambazo watumishi hao wanaweza kupanga."Nawasifu sana wananchi wa Same kwani nyumba nyingi ni za tofali na bati tena ni za kisasa hadi vijijini;Jinsi ambavyo Rais wetu hatoki nchini ili awahudumie wananchi wake kwa karibu.Ndivyo na sisi kwa ngazi zetu tunatakiwa kukaa muda mwingi maeneo yetu ya kazi ili tuwahudumie wananchi wetu kwa karibu"Alisema DC huyo.
Amuagiza kaimu Mkurugenzi Mtendaji kuchukua hatua kwa watumishi ambao watakuwa hawajahamia kwenye maeneo yao ikifika tarehe hiyo na yeye apate taarifa.
Atatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu kati ya kijiji na wananchi.
Ashiriki msaragambo wa ujenzi wa zahanati ya kwanza katika kata hiyo.
Awapa ujumbe wa Mhe.Rais kupitia waziri wa nishati kuwa kabla ya mwezi Disemba 2019,vijiji vyao vitapata umeme wa REA.
Wananchi wampongeza Rais kwa kufufua reli ya Tanga-Arusha inayopita kwenye kata hiyo.Wataalamu waeleza fursa zilizopo serikalini na kuwakumbusha kujitokeza kupiga kura.DC awaeleza jinsi ambavyo ilani ya CCM imetekelezwa kuanzia Taifa hadi kata yao.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.