Washiriki 61 waimba na nyimbo zaidi ya 150 zapatikana Wilayani Same kwa mara ya kwanza.
Nyimbo za kumpongeza Mhe.Rais Dr John Pombe Magufuli na kazi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano zaongoza.
Wizara ya utamaduni yapongeza ubunifu wa maudhui na kuahidi kuendeleza vipaji hivyo.Ndugu Singo ambaye ni Mkurugenzi wa Utamaduni wizarani akimuwakilisha Waziri wa utamaduni na michezo,aliwataka wilaya kufanya bonanza kama hilo kila mwaka na wasanii kulenga kufika kwenye mashindano ya Afrika Mashariki.Aahidi kuwezesha mshindi wa kwanza.
"Tunaamini kati ya waimbaji hawa,wapo akina Diamond,Hamonizer na kina Rose Muhando wa baadaye.Hivyo tutaendelea kuelimisha na kuhabarisha jamii kupitia vipaji vyao".Alisema DC Same.
Washiriki wapongeza kuandaliwa bonanza hili kwani limewezesha kuonesha vipaji vyao ambavyo havikujulikana kabla.Waomba yafanyike kila miezi 6.
Mkomazi wapata balozi wa kuitangaza.KINAPA yaalika kupanda mlima Kilimanjaro.
"Same is not same"
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.